UDSOL YAANDAA KILELE CHA MASHINDANO YA KIMAHAKAMA

::::::::

Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imesema inatarajia kufanya kilele cha msimu wa tatu wa fainali za Mashindano ya Mahakama Igizi (UDSoL).

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Mratibu wa UDSoL, Dkt. Petro Protas, imesema kuwa kilele hicho kitafanyika Juni 4, 2025, katika Ukumbi wa Council Chamber, ulioko katika Kampasi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia saa mbili asubuhi.

Aidha, Dkt. Protas amewataka watu kujitokeza katika kilele hicho, huku TULIA TRUST, AKIPLAW ADVOCATES, FB Attorneys, AfriCorp Attorneys, Tanzania Relief Initiatives na TANAHUT wakiwa sehemu ya wadhamini wa shughuli hiyo.
 



0/Post a Comment/Comments