VIBALI SITA VYATOLEWA USAMBAZAJI GESI ASILIA VIWANDANI, TAASISI


:::::::::::::

Hadi Aprili, 2025 EWURA ilitoa vibali sita (6) vya ujenzi wa mabomba ya kupeleka gesi asilia kwenye viwanda, taasisi, migahawa ya chakula na majumbani. 

Kati ya vibali hivyo, kibali kimoja (1) kilitolewa kwa Kampuni ya PAET kwa ajili ya ujenzi wa bomba la kupeleka gesi asilia kwenye kiwanda cha Aluminium Africa (ALAF) Jijini Dar es Salaam na vinne (4) kwa Kampuni ya TPDC kwa ajili ya kuunganisha gesi asilia kwenye nyumba 451 katika maeneo ya Mnazi Mmoja (Lindi), nyumba 529 maeneo ya Mkuranga (Pwani), Mlimani City Mall na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). 

Aidha, kibali kingine kilitolewa kwa kampuni ya Rashal Energies kwa ajili ya ujenzi wa bomba la usambazaji gesi asilia kutoka eneo la Kisemvule hadi Mbagala.

#Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26

0/Post a Comment/Comments