:::::::
Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Johari Samizi amewataka vijana waliojiunga na mafunzo ya jeshi la Akiba mwaka huu wilayani humo kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo vizuri ikiwa ni pamoja na kuwa wazalendo kwa taifa lao sambamba na kuendelea kuitunza amani iliyopo
Samizi ametoa wito huo katika hafla fupi ya kufungua mafunzo hayo yaliyoambatana na burudani mbali mbali ambapo amewataka vijana hao kuhakikisha unazingatia wanachofundishwa ili waweze kuhitimu na kulitumikia taifa
Kwa upande wake kaimu mshauri wa Jeshi la Akiba wilayani misungwi Japhet Mgeta akisoma taarifa ya mafunzo hayo amesema mafunzo yameanza Aprili 8 mwaka huu ambapo yatachukua miezi 4 na jumla ya vijana waliojiunga ni 109 ambao watapewa mafunzo mbali mbali
Nao baadhi ya vijana waliojiunga katika mafunzo hayo Isack Yahaya na Monica James wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fursa ya katika jeshi hilo huku wakiahidi kuwa wazalendo na kuendelea kuilinda amani iliyopo
Post a Comment