Father Dkt. Charles Kitima
..........
Asema hatutakiwi kuogopa gharama za Kusimamia Haki
Dar. Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amtembelea Father Dkt. Charles Kitima. na kusema kuwa hakika lilikuwa shambulio baya lenye lengo la kudhulumu maisha.
Kupitia mtandao wake wa kijamii Wakili Mwambusj ameandika; 'Mungu ni mwema sana anaendelea vizuri.Huu ni Ujumbe wake kwetu
..Lazima Tuwe Imara kusimamia masuala ya Msingi katika Taifa.
Hatutakiwi kuogopa kulipa gharama katika kusimamia haki na Wajibu wetu kwa Taifa.
Kila Mmoja atalipa gharama kwa kiasi chake na hilo lazima tuwe tayari.
Tunapozungumzia mambo ya Msingi Kitaifa yanayotakiwa kurekebishwa ili uchaguzi ufanyike kwa haki tusiogope kulipa gharama, " amesisitiza rais huyo leo Alhamisi Mei Mosi, 2025.
Post a Comment