:::::::
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inaendesha semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari Mabalozi wa LATRA juu ya kazi na majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka.
Semina hiyo ni ya siku mbili imefunguliwa rasmi na CPA Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA ambapo katika ufunguzi huo amewapongeza wanahabari hao kwa kuwa mabalozi wazuri katika ufikishaji wa habari zinazohusu sekta ya usafiri ardhini kwa watanzania.
Aidha CPA Suluo amewaasa wanahabari hao kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazohusu uchaguzi mkuu na kuepuka habari zinazopotosha jamii pamoja na kuandika kwa umahiri habari zinazohusu sekta ya usafiri nchini.
Semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari Mabalozi inafanyika ukumbi wa Tari- Kibaha Pwani kuanzia Mei 6 hadi Mei 7, 2025 ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo majukumu ya LATRA katika udhibiti usafiri wa barabara, Nafasi ya TEHAMA katika kuboresha huduma za usafiri ardhini, Nafasi ya wanahabari katika kuboresha huduma za usafiri ardhini na Mafanikio ya LATRA katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
*** PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY TORCH MEDIA****
Post a Comment