WAONYWA KUJIHUSISHA NA IMANI ZA KUSHIRIKIANA


 *****

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Magu, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Haji Makame, amewataka wananchi kuachana na imani za kishirikina ambazo zimekuwa chanzo kikuu cha mauaji na migogoro ya kijamii.

SSP Makame ametoa wito huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kisamba, kata ya Lubugu, wilayani humo, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kutoa elimu ya ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia uhalifu.

Aidha, amewataka viongozi wa serikali za vijiji kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia mauaji yanayotokana na imani za kishirikina, migogoro ya ardhi na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Mmoja wa wananchi, Paskazia Kibuga, amewataka wenzake kuachana na imani hizo potofu akisema, “Kifo hakiepukiki, mchawi haonekani. Naomba jambo hili kwenye kijiji chetu liondoke kabisa, linaniudhi.”

Kwa upande wake, Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lwele Mpina, ameonya vikali dhidi ya watu wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe na albino, akisema kuwa yeyote atakayejihusisha atakumbana na mkono wa sheria.





0/Post a Comment/Comments