.......
Dar. Mdogo wa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amefariki dunia ghafla jijini Dodoma muda mfupi baada ya kushuhudia kaka yake akiwasilisha leo makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka 2025/2026.
Ally Hamidu Aweso, aliyefariki dunia ghafla alfajiri ya leo Ijukaa Mei 9,2025 jijini Dodoma.
Ally Aweso alikuwa amewasili jijini Dodoma akitokea Tanga kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Bunge kilichofanyika jana Mei 8 2025, kwa lengo la kumuunga mkono kaka yake wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kupitia account yake ya Instagram, Waziri Aweso alitoa tangazo la kifo cha mdogo wake na kusema amepokea taarifa ya msiba huu wa kushtukiza mara tu baada ya kuhitimisha hoja yake Bungeni na kufanikisha kupitishwa kwa makadirio ya bajeti ya wizara ya Maji.
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa Mhe. Waziri katika eneo la Ilazo, karibu na Saanan Hotel, jijini Dodoma.
Ratiba ya kuusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Pangani, Tanga kwa ajili ya maziko imepangwa kufanyika leo saa 11:00 jioni, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 10 Mei 2025 majira ya saa 7:00 mchana.
Torch Media Tunatoa pole kwa familia ya Mhe. Aweso, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.
Inna Lillahi wa inna ilayhi raj'un.
Post a Comment