𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗜𝗡𝗔𝗧𝗛𝗔𝗠𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗢 𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗠𝗨



 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Walimu katika elimu na malezi ya watoto katika nyanja mbalimbali za maisha.

Waziri Mkenda amesema hayo Juni 14, 2025 jijini Dar es Salaam katika Hafla ya Utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Shindano la Tatu la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Msingi na la Kwanza kwa Walimu wa Sekondari.

"Kila mmoja wetu ana historia chanya na kumbukumbu ya mwalimu ama walimu walioshawishi maendeleo yetu ya elimu katika nyanja mbalimbali" Alisema Waziri huyo.

Prof. Mkenda amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati anazindua Sera ya Elimu alisisitiza kuwa Serikali inathamini mchango wa Walimu katika mageuzi ya elimu, aliwahimiza kufanya kazi kwa weledi kuhakikisha Taifa linapata wahitimu mahiri wenye ujuzi stahiki.

Waziri Mkenda aeishukuru Benki ya Dunia kwa kufadhili Shindano hilo muhimu chini ya Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).










0/Post a Comment/Comments