Na Ester Maile Dodoma
Benki ya CRDB imetumia kiasi cha Sh130 milioni kununua vifaa vya michezo kwa ajili ya Bonanza la Bunge linalotarajiwa kufanyika mwisho wa wiki.
Benki hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa Grand Bunge Bonanza linalohusisha timu za wabunge imetumia fedha hizo kununua vifaa vya michezo ili kuleta hamasa kwa wabunge kushiriki katika michezo na jamii.
Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo June 21, 2025 ambapo michezo kumi na mmoja itachezwa kati ya wabunge na taasisi mbalimbali.
Mwenyekiti wa Bonanza hilo, Festo Sanga amesema leo June 18,2025 kuwa bonanza hilo litahitimisha shughuli za Bunge kwa kipindi cha miaka mitano
Sanga amesema pamoja na kuwa michezo inasaidia kuimalisha mwili lakini pia hujenga Taifa imara na hamasa kati ya wabunge na taasisi mbalimbali.
Sanga ametoa wito kwa wanahabari, vyuo mbalimbali na taasisi kushiriki katika Bonanza hilo na kuzitaka taasisi zingine kuiga mfano wa benki ya CRDB kwa kuandaa mashindano hayo.


Post a Comment