..................
Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Juni 16, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, huku Mahakama ikimpa onyo kali kwa kutamka maneno bila ruhusa ukumbini.
Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, ametoa uamuzi huo leo Juni 2, 2025 wakati shauri hilo lilipotajwa ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na jopo la mawakili wakiongozwa na Nassoro Katuga, huku utetezi ukiwakilishwa na Mpale Mpoki.
Katika maelezo yake, Hakimu Kiswaga alisema hakuna ubishi kuwa mshtakiwa alitamka maneno ya “No reform, no election” akiwa mahakamani, kauli iliyotafsiriwa na upande wa Jamhuri kuwa ni ya kudharau Mahakama.

“Mara tu Mahakama inapokaa, inakuwa kamili kwa mujibu wa kifungu cha 6(c) hivyo hakuna aliyepaswa kuongea bila ruhusa na mshtakiwa hakupaswa kutoa kauli hiyo,” alisema Hakimu Kiswaga.
Aidha, Mahakama ilisisitiza kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote – iwe ni mshtakiwa au wasikilizaji wa kawaida – kuzungumza bila ruhusa ya Mahakama. “Hatua hiyo ni muhimu kuhakikisha Mahakama inafanya kazi kwa kufuata sheria na si mihemko ya mtu binafsi,” alisema Hakimu.
Katika kesi hiyo, Lissu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam, ambapo alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwa lengo la kushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, pamoja na kumshinikiza kiongozi mkuu wa serikali.
Post a Comment