Na Gordon Kalulunga
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya ndugu Ndele Mwaselela, amewahimiza idara ya UVCCM katika vyuo na vyuo vikuu kujibu hoja za wapinzani wanaopotosha taarifa za miradi ya maendeleo katika mitandao ya kijamii.
Ameyasema hayo leo Juni 13,2025 Jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la Seneti ya Elimu ya watu wazima.
Pamoja na mambo mengine M-NEC Mwaselela amewachangia kiasi cha Shilingi Milioni Moja, Laki Mbili na Elfu Sitini 1,260,000 kwa ajili ya vifaa vya TEHAMA vitakavyowawezesha kujibu hoja za upotoshaji na kueleza miradi iliyotekelezwa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwaselela amesisitiza kuwa chama chao kitashinda kwa kupigiwa kura na watanzania kutokana na miradi chanya iliyotekelezwa na serikali.
"Kazi yetu kubwa kuonesha kazi zilizofanywa na serikali chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan na kujibu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu mitandaoni na ukweli usiopingika ni kwamba CCM tutashinda kwa kupigiwa kura maana kazi zilizofanywa zinaonekana" amenukuliwa kiongozi huyo.



Post a Comment