RAIS SAMIA ATEMBELEA MRADI WA REA SIMIYU

.............

Rais wa Samia Suluhu Hassan ametembelea mradi wa nishati safi ya kupikia wa shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu iliyopo Bariadi mkoani humo.

Rais Samia ambaye yuko mikoani Simiyu, ameoewa maelezo na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akifungua shule hiyo Jumanne Juni 16, 2025.

Mradi huo unahusisha usimikaji wa mfumo wa kupikia kwa kutumia gesi yaani LPG, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hivyo kuchangia katika utunzaji wa mazingira na kulinda afya ya wanafunzi na walimu.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ufadhili wa kiasi cha Sh14 milioni kwa ajili ya ujenzi na usimikaji wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika shule hiyo.




 

0/Post a Comment/Comments