.......,...
Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, amefariki dunia.
Rais Lungu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68.
Taarifa za kifo cha Rais Lungu zimedhibitishwa na familia yake leo Alhamisi, June 5, 2025.
Kupitia video fupi, binti yake Lungu, Tasila, amesema kuwa Rais huyo wa zamani ambaye alikuwa “chini ya uangalizi wa kitabibu katika wiki za hivi karibuni”, alifariki katika hospitali moja huko Pretoria Afrika Kusini saa 12:00 alfajiri hii leo.
Lungu aliiongoza Zambia kwa miaka sita kuanzia 2015, hadi aliposhindwa katika uchaguzi wa 2021 na Rais wa sasa Hakainde Hichilema kwa tofauti kubwa ya kura.
Post a Comment