SERIKALI KUNUNUA MBOLEA NA KUWAGAWIA WAKULIMA


..............

Na Ester Maile Dodoma 

Dola milioni Mia moja na themanini za wekezwa katika kiwanda cha uzalishaji mbolea kilichopo Nala jijini Dodoma. 

Hayo yameelezwa leo 11 June 2025 na Waziri wa Kilimo Husein Bashe wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari akitoa taarifa kwa umma juu ya siku ya uzindunzi wa kiwanda cha uzalishaji mbolea ITRACOM FERTILIZER LIMITED

Amesema hadi sasa kiwanda cha uzalishaji mbolea (ITRACOM) fertilizer Limited kimeanza kuzalisha na mbolea zipo sokoni pia kiwanda hicho kitazalisha na choka kwa ajili ya mashambani .

Hata hivyo amesema serikali itanunua Tani laki mbili za mbolea za viwanda vya ndani na kusambaza kwa wakulima ambao hawatumii mbolea.
 

0/Post a Comment/Comments