SERIKALI YAMUONYA ALIYESAMBAZA UZUSHI KUHUSu VVU

......................

Wizara ya Afya imesikititishwa na taarifa ambayo imesambazwa kwenye mtandao  ikimuonyesha mtu anayejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi kwa jina la Mentor Chery akieleza kuwa dalili mojawapo ya kuwa na virusi hivyo ni mtu kuwa na vidoti vyeusi katika dole gumba la mguu hadi kisigino.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,imesema hatua kali za Sheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yoyote atakayetoa na kusambaza taarifa zinazopotosha jamii.

 Aidha Wizara imeiasa jamii kupuuza  taarifa hizo na wale wote wanaotaka kukua Hali zao Maambukizi ya  Virusi vya UKIMWI wafike katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili kupima na kutambua Hali zao.


Taarifa hiyo imesema mtu huyo ameenda mbali zaidi na kuiasa jamii hasa walio katika uhusiano wachunguze wenzi wao wasiojua hali zao za maambukizi ya Virusi hivyo na endapo watabaini hayo ni wazi kuwa wenzi hao wameathirika kwa kuwa wenye ugonjwa huo nyao zao haziwi nyeupe.

Katika hatua nyingine Wizara imetoa onyo Kwa watu wote ambao si wataalamu wa Afya kujiepuaha kutoa taarifa za Afya huku wakijua kuwa hawana ueledi au taaluma ya kufanya hivyo.

0/Post a Comment/Comments