TEKSI ZA MTANDAONI ZAVUTIA AJIRA MPYA

::::::

Arusha, Tanzania 

 Mabadiliko ya ajira kutoka kazi za ofisini kwenda kwenye sekta ya usafirishaji kwa njia ya mtandao (ride-hailing) yameendelea kuwa njia mbadala kwa baadhi ya viinjana wanaotafuta kipato chenye uhuru zaidi wa muda na fedha.

 Akizungumza jijini Arusha mmoja wa wanaufaika wa huduma ya usafirisshaji ya bolt Laurence Mollel amesema kuwa Mwaka 2021, alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya bima jijini Arusha aliacha kazi yake rasmi na kuanza kutoa huduma ya usafiri kwa kutumia gari alilolinunua kwa kutumia akiba yake,alijiunga na jukwaa la usafirishaji la InDrive, ambapo alifanya kazi kama dereva kwa muda mfupi kabla ya kuongeza gari la pili na kuanza kuajiri madereva.

Baada ya kuingia kwa huduma ya Bolt katika soko la Arusha, Mollel aliongeza wigo wa kupata wateja na kupanua huduma zake kwa kununua gari aina ya Toyota Alphard kwa ajili ya kuhudumia wasafiri wa uwanja wa ndege na watalii.

 Kwa mujibu wa tovuti ya Paylab.com, madereva wa teksi nchini Tanzania hupata kati ya Shilingi 651,000 hadi Shilingi 1.5 milioni kwa mwezi, kiwango kinachozidi wastani wa mshahara wa karani wa ofisini. Takwimu hizi zinaonesha ukuaji wa fursa za kipato katika sekta ya ride-hailing nchini.

0/Post a Comment/Comments