KITUO CHA BIASHARA EACLC UBUNGO KUZINDULIWA AGOSTI 2 NA RAIS SAMIA

:::::::
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha Kibiashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo, Dar es Salaam, Agosti 2, 2025. 

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneneo Maalumu ya Kiuchumi (TISEZA), Gilead Teri amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kituo hicho ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia ukuzaji wa mauzo ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi. 

Amesema kituo hicho kitakapoanza, Tanzania inatarajia kunufaika na mapato ya kila mwaka yanayokadiriwa kuwa dola milioni 10 za Marekani kila mwaka. 

Kuhusu madai kuwa kituo kitazorotesha biashara eneo la Kariakoo, Teri amesema biashara katika eneo hilo zitaendelea kushamiri kutokana na kituo hicho kutokuwa na ushindani wowote na Kariakoo. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki -EACLC, Catherine Wang amewataka wafanyabiashara Nchini kuchamkia fursa ya uwepo wa kituo hicho ili kujikwamua kiuchumi.

Kituo hicho cha kisasa cha uwekezaji cha biashara na usafirishaji cha Afrika Mashariki kina maduka zaidi ya 2,060 na na kimetoa ajira za moja kwa moja 15,000 na 50,000 zisizo za moja kwa moja.
 











Picha zote na James Salvatory Torch Media

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments