WAGOMBEA WALIOKOSA NAFASI WAENDELEE KUWA WAVUMILIVU KWENYE CHAMA _MAKALLA

:::::::

Na Ester Maile 

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla amewaomba watia nia katika nafasi za ubunge,viti maalum pamoja na madiwani kuendelea kuonesha ushirikiano ndani ya chama hata kama wamekosa nafasi ya kupita.

CPA Amos Makalla amesisitiza kuwa kwa wale wote ambao hawajafakiwa kupata nafasi waendelee kuwa watulivu na kuonesha ushirikiano huku akibainisha kuwa chama hicho kina nafasi nyingi hivyo wanaweza kuomba hizo nafasi zingine kwa sababu wamedhubutu.

Hayo ameyasema leo Julai 29 ,2025 katika ukumbi wa mikutano wa CCM makao makuu Jijini Dodoma alipokuwa anatangaza majina ya watia nia katika nafasi za Ubunge ,Viti maalum na makundi mengine ambayo yamefanikiwa kupitishwa na kamati kuu ya Halmashauri ya chama cha mapinduzi iliyoketi jana Julai 28, 2025.

Hata hivyo katika kuangaza majina hayo baadhi ya Majina ya vigogo yamerudi baada ya kushindwa kupata nafasi mwaka 2020 akiwepo aliyekuwa Mbunge wa Sengerema William Ngeleja,Steven Masele na vigogo wengine.

Wakati huohuo katika mchujo huo yapo pia majina ya Vigogo waliojizoelea Umaarufu bungeni kwa mwaka 2020/2025 ambapo wameshindwa kupenya akiwepo Askofu Gwajima(Kawe),Luhaga Mpina(Kisesa) pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba.

Itakumbukwa kuwa kwa mujibu wa ratiba ya ya tume huru ya uchaguzi itakapofika tarehe 14 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 kutakuwa zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani.



 

0/Post a Comment/Comments