WATAALAMU WASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA AI

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga (kushoto),akiwa Dkt George Mulamula (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Datavera Bilal Hmede katika siku ya pili ya Jukwaa la Akili Unde la Tanzania 2025 ambalo limefanyika kuanzia Julai 28-29 mwaka huu jijini Dar es salaam

......................

NA MUSSA KHALID

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga amewasisitiza watanzania hasa vijana kutumia fursa ya uwepo wa Akili Unde kwa kutegeneza bunifu mbalimbali zitakazosaidia nchi kuwa shindani kiuchumi.

Dkt Mwasaga ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akziungumza na waandishi wa habari katika siku ya pili ya Jukwaa la Akili Unde la Tanzania 2025 ambalo limewakutanisha wadau kutoka mataifa mbalimbali.

Aidha Dkt Mwasaga amesema kuwa kutokana na Akili Unde kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi hivyo wamejadili kuhusiana na maadili ili kujenga kizazi kilichobora ambacho kitatumia mfumo huo kwa faida.

‘Tunaangalia maadili katika Akili Unde kwa sababu saa hivi inakuwa na uwezo fulani kwa ajili ya kutoa maamuzi yenyewe na kama inaweza wote tunafahamu masuala ya maadili ni ya msingi hivyo hii mifumo tujue kwamba inafanya kwa kuangalia tamaduni zetu,mila zetu na kufata sheria zetu za Tanzania”amesema Dkt Mwasaga

Akizungumza katika Jukwaa hilo,Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Tabora Dkt Adam Mambi amesema matumizi ya Akili Unde yamekuwa yakirahisisha katika utendaji wa haki kwenye mahakama za Tanzania.

Amesema kuwa takriban Mahakama 11 za Mahakama kuu za Tanzania wameweza kuweza kuweka mfumo wa Akili Unde ambao unaweza kurikodi wakati shahidi au mwanasheria anaongea halafu baadae sauti inaweza kugenuzwa kuwa kama maneno.

Jukwaa hilo ambalo limeanza Jana na kuhitimishwa leo limewaleta pamoja wataalamu wa teknolojia, watunga sera, wawakilishi wa sekta binafsi, na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujadili mwelekeo wa AI nchini Tanzania ambapo umelenga kuweka msingi wa sera jumuishi na endelevu zitakazoiwezesha Tanzania kuongoza katika matumizi salama na jumuishi ya teknolojia ya Akili Bandia barani Afrika.

 

0/Post a Comment/Comments