Katika kipindi cha miezi 14 tu, zahnati ya Mihama katika Manispaa ya Ilemela imehudumia wagonjwa wa nje zaidi ya 2,000, Watoto 78 wamezaliwa hapo na watoto zaidi ya 50 kutoka kaya za walengwa wa TASAF wanapata huduma za klinikina kutimiza masharti ya afya katika kupata ruzuku za TASAF.
Ikiwa imejengwa kwa gharama ya Sh 241.9 kwa kuibuliwa na Mitaa miwili ya Mihama na Jiwe Kuu ambapo Mihama waliibua mradi wa jingo la wagonjwa wan je lneye thamani ya Sh 111 milioni na Jiwe Kuu nyumba vyumba vitatu vya watumishi yenye thamani ya sh milioni 129.9.
Zahanati hiyo yenye vifaa vya kisasa vinavyotolewa na Serikali imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mitaa ya Jiwe Kuu na Mihama ambao hupata matibabu bure.
“Inabidi tuipongee sana Serikali inayoongozowa na Rais Dr. Samia suluhu Hassan kwa mafanikio haya. Vifaa vilivyopo hapa pamja na majengo yake ni vya hadhi ya juu sana,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray alipotembela zahamati hiyo pamoja na menejimenti ya TASAF.
Post a Comment