Mjumbe Maalumu wa Masuala ya wanawake, Amani na Usalama, Barani Afrika Balozi Liberata Mulamula ameungana na wananchi kupiga kura(kutiki) kumchagua Rais, mbunge na diwani huku akisifu utaratibu na utulivu wa wananchi kupiga kura.
Balozi Mulamula amejitokeza kutiki mapema leo katika kituo Cha Kupiga kura Cha Maliasili Mbezi Jogoo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
"Kituo chetu cha Maliasili Mbezi Jogoo, kimefunguliwa kwa wakati. Kila kitu kimeonekana kimepangiliwa vizuri. Mimi nimefika kituoni saa tatu asubuhi. Watu wamejitokeza na kwa muda niliokuwa kituoni watu walikuwa wakiongezeka, kwa kweli upigaji kura umeanza vizuri kwa utulivu na weledi," alieleleza
Balozi Mulamula aliwasisistiza wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowakata watakao waongoza katika safari ya miaka mitano kwa maendeleo.
.jpg)

Post a Comment