FARU WEUSI NANE ULINGONI LEO UBINGWA WA AFRIKA KANDA YA 3 NAIROBI

:::::::::::

Mabondia nane wa kikosi cha timu ya ngumi ya Tanzania almaarufu kama Faru Weusi watapanda ulingoni  leo jijini Nairobi, Kenya katika mashindano ya Afrika Kanda ya tatu.

Wachezaji hao wataongozwa na wakongwe Kassim Mbundwike ambaye ni mshindi wa medali ya Shaba jumuiya ya madola Birmingham 2022 atakayepambana na Mazongo Anderson kutoka DR Congo katika uzani wa 'Light middleweight' 71kg huku George Mbonabucha dhidi ya Kumbo Mwinyi kutoka Kenya B na Ezra Paul akipimana ubavu na Washington Wandera kutoka Kenya A.

Jumla ya mapambao 32 yatapiganwa leo katika uwanja wa ndani wa Kasarani katika awamu mbili tofauti yaani  mchana na jioni.

Awamu ya kwanza ya mapambano yataanza saa tisa alasiri
na awamu ya pili itaanza saa mbili usiku
Ratiba kamili ni kama ifuatavyo:

Mchana
Light fly 48 kg
1.  Juma Athumani vs Abednego Kyalo (Kenya A)

Light weight 60 kg
2.  Ezra Paulo vs Washington Wandera (Kenya B)

Welterweight 67 kg
3.  Shafii Mbaraka vs Lendoye Arthur (Gabon)

Jioni
Fly weight 51 kg
4.  Aziz Chala vs Tulembekwa Zola (DR Congo)

Featherweight 57 kg 
5.  George Mbonabucha vs Kumbo Mwinyi (Kenya B)

Light welterweight 63.5 kg 
6.  King Lucas vs Engo Mba Laurent (Gabon)

Light middleweight 71kg
7.  Kassim Mbundwike vs Manzongo Anderson 

Heavyweight 92 kg 
8.  Emmanuel Augostino vs Abdoul Ringo (Uganda)

 




0/Post a Comment/Comments