Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza mwelekeo wa mvua za msimu wa Novemba 2025 hadi Aprili 2026 kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka, ikidai kuwa msimu huo utatawaliwa na vipindi virefu vya ukavu pamoja na mtawanyiko wa mvua usioridhisha katika maeneo mengi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC), amesema mvua zinatarajiwa kuanza mwezi Novemba na kumalizika kati ya Aprili na Mei 2026, lakini hazitakuwa za kuridhisha katika maeneo mengi.
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni pamoja na mikoa ya magharibi (Kigoma,
Tabora, Katavi), kanda ya kati (Singida, Dodoma), nyanda za juu kusini
magharibi (Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa), kusini (Ruvuma), ukanda wa
pwani ya kusini (Lindi, Mtwara), pamoja na kusini mwa Morogoro.Amesema mvua hizo zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya nne ya
mwezi Aprili na wiki ya kwanza ya mwezi Mei 2026 katika maeneo mengi yanayopata
mvua za msimu.
Dk. Chang'a amesema ongezeko la mvua linatarajiwa katika
kipindi cha nusu ya pili ya
msimu unaonza mwezi Februari mpaka Aprili, 2026
ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwezi Novemba, 2025 mpaka Januari, 2026.
Pamoja na mvua hizo kuwa za wastani hadi chini ya wastani,
Dk. Chang'a ametoa angalizo uwepo wa matukio ya vipindi vya mvua kubwa yanaweza
kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za chini ya wastani.
PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY TORCH MEDIA










Post a Comment