MWANDISHI WA TORCH MEDIA ASHINDA TUZO ZA TMA


 :::::::::::::

Mwandishi wa habari kutoka Torch Media, James Salvatory,  ametunukiwa tuzo ya umahiri kwa kazi zake kuhusu hali ya hewa.

Tuzo hiyo imetolewa leo Alhamisi, Oktoba 16, 2025, na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wanahabari katika kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi na taarifa za hali ya hewa.

Salvatory ameibuka mshindi wa tatu katika kundi la habari za mtandaoni na kupokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Jaji Mshibe Bakari.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Salvatory amesema ni heshima kubwa kutambuliwa kitaaluma, na kwamba ushindi huo ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi zaidi.

Ameongeza kuwa uandishi wa habari za hali ya hewa ni eneo linalohitaji umakini na uelewa wa kina, hivyo ataendelea kujifunza na kuboresha kazi zake kwa manufaa ya jamii.













0/Post a Comment/Comments