SHIRIKA LA POSTA LAADHIMISHA SIKU YA POSTA KIVINGINE

Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dar es salaam  Paul Mshanga akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo wakati wa madhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila Oktoba 9 ya kila mwaka.Msimamizi wa Biashara Shirika la Posta Mkoa wa Dar es salaam Hamisi Swedi akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo wakati wa madhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila Oktoba 9 ya kila mwaka.Wafanyakazi wa Shirika la Posta Dar es salaam wakisheherekea madhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila Oktoba 9 ya kila mwaka ambayo yamefanyika katika ofisi za Shirika hilo.(picha zote na Mussa Khalid)

....................

NA MUSSA KHALID

Shirika la Posta Tanzania limeendea kuhakikisha linatoa huduma bora na salama za usafirishaji kwenda zaidi ya nchi wanachama 190 wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) na hivyo kuwawezesha Watanzania kushiriki kwa ujasiri katika biashara na mawasiliano ya kimataifa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dar es salaam  Paul Mshanga wakati akizungumza na wafanyakazi na wadau kutoka taasisi mbalimbali kwenye madhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila Oktoba 9 ya kila mwaka

Mshanga amesema kuwa shirika hilo kwa sasa limebadilika na Mafanikio hayo yanadhihirisha kuwa Posta ni zaidi ya usafirishaji wa barua, bali ni kichocheo cha biashara, huduma za kifedha na maendeleo ya kitaifa.

Posta ikiwa na ofisi zaidi ya 400 na vituo vya uwakala zaidi ya 1,200 vilivyosambaa nchi nzima, imekuwa ikihudumia wateja zaidi ya milioni 5 kila mwaka iwe ni mkulima anayesafirisha mazao ndani na nje ya nchi kupitia Post Cargo, mwanafunzi wa chuo kikuu anayewasilisha maombi ya udhamini wa masomo ya kimataifa kupitia EMS, au mjasiriamali”amesema Mshana

Kwa upande wake Msimamizi wa Biashara Shirika la Posta Mkoa wa Dar es salaam Hamisi Swedi ametoa wito kwa wananchi, wafanyabiashara na wadau kuendelea kutumia huduma za Shirika hilo kama injini ya biashara, mshikamano wa kijamii na maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa Kupitia programu za kufikia vijijini na upanuzi wa vituo vya kifedha na huduma nyingine katika wilaya ambazo hazijafikiwa kikamilifu, Posta imeendelea kuhakikisha hata vijiji vya pembezoni vinaunganishwa na mtandao wa kitaifa wa posta sambamba na wito wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) wa kutoa huduma za posta bila kumwacha yeyote nyuma.

Aidha ameeleza kuwa Kaulimbiu ya mwaka 2025 inaendana kwa kina na mwelekeo wa kimkakati wa TPC unaojengwa juu ya nguzo ya biashara mtandao, ubunifu wa kidijitali katika kuboresha huduma pamoja na huduma bora kwa mteja.

‘Kwa kujikita katika dira ya UPU ya “#Posta kwa watu: huduma za kitaifa zinazoenda kimataifa,” Posta itaendelea kujihakikishia nafasi yake kama  mhimili wa kuunganisha Tanzania na dunia’ameeleza Swedi wakati akisoma hotuba

Nao baadhi ya wateja wa Shirika la Posta Tanzania ,Crispin Mathew kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania pamoja na Maula Victor mwakilishi kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wamelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kutoa huduma bora na hivyo wameahidi kuendeleza ushirikiano.

Kwenye Maadhimisho hayo pia kumefanyia zoezi la utoaji wa vyeti na zawadi kwa wadau mbalimbali wakiowemo wanafunzi ambao wamefanya vizuri yamekwenda sambamba na Kauli mbiu isemayo  “Posta kwa Watu: Huduma za kitaifa zinazoenda Kimataifa,” ambayo  ikumbusha dhamira ya kudumu ya posta ya kuunganisha jamii katika ngazi za ndani huku ikivuka mipaka ya dunia.

0/Post a Comment/Comments