TUNACHUNGUZA POLEPOLE KUTEKWA - POLISI


....................
Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa, bado linaendelea kumsubiri Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai huku pia likikiri kuona taarifa ya kutekwa kwake na wameanza uchunguzi.

“Ndg. Humphrey Polepole alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa Sheria za nchi aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao ya Kijamii làkini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa Sheria.

“Jeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa, tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake”-




 

0/Post a Comment/Comments