WAKILI MWANAISHA MNDEME WA ACT-WAZALENDO AENDELEA NA KAMPENI KIGAMBONI

........................

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Wakili @mwanaisha__mndeme ameendelea na kampeni zake kwa mtindo wa mtaa kwa mtaa,kwenye mitaa iliyopo Kata ya Kibada na Kata ya Kigamboni, huku akipata mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.

Katika kamepeni hiyo ya mtaa kwa mtaa Mwanaisha amewaeleza wananchi sera za ACT Wazalendo na kueleza mipango yake ya kuleta maendeleo katika maeneo ya uvuvi,vivuko ,elimu, afya, miundombinu ya barabara na ajira kwa vijana. Aliahidi kuwa sauti ya wananchi wa Kigamboni itasikika Bungeni endapo watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo

Kampeni za Wakili Mndeme zinaendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kigamboni,ikiwa ni kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025






0/Post a Comment/Comments