BALOZI MULAMULA- MICHEZO NI MUHIMU KWA AFYA,ELIMU NA MAENDELEO


:::::::::

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Africa kuhusu Wanawake Amani na Usalama, Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Tamasha la Michezo la 'Ladies First' la wanariadha wanawake huku akisisitiza umuhimu michezo katika kujenga afya njema na kuchochea elimu na maendeleo.

Akizungumza katika Tamasha hilo, lililofanyika Jijini Dar es Salaam kukusanya wanamichezo mbalimbali likifadhiliwa na Shirika la Japan Maendeleo (JICA).

"Nimefurahi kushiriki Tamasha hili muhimu la wanariadha wanawake, lenye lengo la kuhamasisha michezo kama sehemu ya kujenga afya bora, kuhamasisha elimu na maendeleo ya jamii.Nivyema tukazingatia hili kwa kila mmoja kulinda afya zetu dhidi ya maradhi na kuhamasisha maendeleo kwa kila mmoja,"alisema.

Tamasha hilo liliongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma akiambata na viongozi wengine wakiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo, Neema Mshita na Rais wa Shirikisho la Wanariadha Tanzania, . Rogath Stephen, Col. Jumaa Ikangaa, Balozi wa Heshima wakilishi wa JICA nchini Tanzania, Hiroshi Ara.

Tamasha hilo, linalofanyika kila mwaka lilianzishwa na mwanariadha maarufu mkongwe, Juma Ikangaa kwa ufadhili wa JICA kuhamasisha wanawake kushiriki michezo kwa afya na elimu na maendeleo.

00000

0/Post a Comment/Comments