TAMKO LA JESHI LA POLISI KUHUSU WATU WANAODAIWA KUHUSIKA KURATIBU MAANDAMANO

Mnamo Novemba 12, 2025, Jeshi la Polisi Tanzania lilitoa taarifa kwa umma likieleza kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusu watu wanaodaiwa kupanga na kuhamasisha maandamano kupitia makundi ya mawasiliano ya mtandaoni, hususan kupitia WhatsApp.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, uchunguzi wa polisi umebaini uwepo wa watumiaji wa namba mbalimbali waliopo nchini na nje ya nchi wanaodaiwa kushirikiana kupanga vitendo vya uvunjifu wa amani kwa mwavuli wa maandamano ya amani.

Miongoni mwa watu waliotajwa katika uchunguzi huo ni:-
1. Yunus Karsan raia wa Tanzania, Simu Namba, +447360921291
2. Said Khamis raia wa Tanzania, Simu Namba +255713213476
3. Olipa Manyama raia wa Tanzania, Simu Namba +255769353620
4. Abdulrahiman Juma raia wa Tanzania, Simu Namba +255745989395
5. Juma Abdallah raia wa Tanzania, Simu Namba +255788981512

ambao wanadaiwa kutumia namba ya simu kupanga, kuratibu na kuhamasisha maandamano kupitia mawasiliano ya mtandaoni.
Jeshi la Polisi linawataka watajwa hapo juu wajisalimishe mara moja katika kituo chochote cha polisi popote walipo.

Aidha, Jeshi la Polisi bado linaendelea kuwatafuta watu wengine wanaohusishwa na mawasiliano hayo, huku majina yao mengine yakisalia kutotajwa kwa sababu za kipelelezi. Polisi walisisitiza kuwa mara uchunguzi utakapokamilika, hatua za kisheria zitafuata.

Jeshi la Polisi, linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na makundi ya mawasiliano mtandaoni yanayoendeshwa na watu waliopanga na wanaendelea kupanga kufanya uhalifu nchini kwa mwavuli wa maandamano ya amani au kwasababu nyingine yeyote ile kwani huo ni uhalifu na hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa yeyote yule atakayebainika.


0/Post a Comment/Comments