:::::::::::
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali itanunua ndege mpya nane zitakazoongeza uwezo wa ATCL kupanua safari za ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za uendeshaji ili kuongeza tija.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa ATCL, kilichofanyika Jijini Dar es salaam, Prof mbarawa amesema ujio wa ndege hizo unapaswa kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia, kuondoa safari zisizo na faida na kuhakikisha ndege zinatumika kwa ufanisi.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mha. Peter Ulanga, amesema ujio wa ndege mpya nane zitaimarisha huduma na ushindani wa shirika na kubainisha kuwa mwongozo na sera madhubuti za Wizara zimeendelea kuwezesha ATCL kupanua mtandao wake wa safari za Kitaifa na Kimataifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL Prof.Neema Mori, amepongeza mkutano huo na kusema kuwa Bodi itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ili kuhakikisha Shirika linakuwa imara, lenye tija na ushindani katika soko la ndani na nje.
Kikao hiki cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa ATCL kimewakutanisha menejimenti na wawakilishi wa wafanyakazi kujadili masuala muhimu ya uendeshaji, ustawi wa wafanyakazi, uboreshaji wa huduma, na mikakati ya kuongeza ufanisi wa shirika. Kupitia majadiliano.









Post a Comment