Benki ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival kuandaa matamasha ya watoto kwa lengo la kuwawezesha kukuza maarifa katika masuala ya fedha.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema lengo la ushirikiano huo ni kutoa elimu ya fedha kwa vijana na kuongeza ujumuishi wa huduma za fedha katika jamii.

Sambamba na udhamini huo, Benki ya CRDB itatoa ufadhili wa masomo kwa washindi wanne watakaopatikana katika matamasha mawili yatakayofanyika tarehe 20 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam na tarehe 27 Desemba 2025 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kids’ Holiday Festival, Geraldine Mashele. Kupitia ushirikiano huu, Benki ya CRDB inalenga kuunganisha burudani na elimu kwa vijana kwa kutoa elimu ya fedha, uwekezaji na akiba kwa kundi la vijana ambalo ni msingi wa maendeleo ya taifa letu.
.jpg)

Post a Comment