CHATO TEACHERS SACCOS KUKOPESHA ZAIDI YA MIL. 775*

Katibu wa Chato teachers Saccos, Pius Katani, akitoa ufafanuziKushoto ni Katibu wa Saccos, Pius Katani,(katikati) mwenyekiti wa Saccos, Petro Rwegasira

***********

 CHATO

"Maendeleo ya kweli hayawezekani bila mabadiliko ya kifikra, na wale ambao hawawezi kubadilika namna wanavyofikiri hawawezi kubadili chochote" George Bernard Shaw alipata kuandika.

Kutokana na ukweli huo unaweza kusema wazi kuwa kazi nzuri, fikra yakinifu na mabadiliko makubwa ya mwenendo wa Chama cha ushirika wa kuweka na kukopa cha walimu chato (Chato Teachers Saccos) inapaswa kuungwa mkono kutokana na hatua kubwa za kimaendeleo kwa kipindi cha mwaka 2025/26.

Hatua hiyo inatokana na Chama hicho kuongeza kiwango cha mawekesho ya fedha za wanachama wake kwa kiasi cha shilingi 1,278,397,350 sawa na ongezekao la aslimia 9 ukilinganisha na kiasi cha 1,180,400, 556 mwaka 2024.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho mwaka 2025, Katibu wa Teachers Saccos, Mwl. Pius Katani, amesema kwa mwaka 2026 wanakusudia kukopesha kiasi cha shilingi milioni 774,000,000 ukilinganisha na kiasi cha milioni 662,157,000 kilichokopeshwa mwaka 2025.

Aidha Chama hicho kimefanikiwa kukusanya zaidi ya sh. milioni 130.5 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali kati ya kiasi cha sh. milioni 196.2 zilizotolewa kwa wanachama ikiwa ni sawa na aslimia 67 ya makisio yaliyotarajiwa mwaka 2025.

Katani, amesema katika kuimalisha uchumi wa taasisi, Chama hicho kimelazimika kubana matumizi yake na kutumia kiasi cha shilingi milioni 79.6 kati ya milioni 188.7 zilizotarajiwa kutumika katika kipindi cha mwaka 2025.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Chama hicho, Mwl. Petro Rwegasira, amesema Chama hicho kimekuwa mkombozi mkubwa wa watumishi wa umma wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari.

Kadhalika amesema kutokana na mwenendo mzuri wa Saccos hiyo, wanachama wameendelea kujiunga hadi kufikia 642, mwaka 2025.

Kwa mujibu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa vyama vya ushirika nchini (Coasco) iliyotolewa na kaimu mkurugenzi mkuu CPA J. J. Mugeta, Chato Teachers Saccos kimepata hati safi kutokana na uendeshaji na usimamizi mzuri wa fedha za wanachama wake.

Kwa upande wake, Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Geita, Doreen Mwanri, amewataka wanachama wa Chama hicho kuendana na mabadiliko ya uendeshaji wa Saccos hiyo kwa kuzingatia waraka wa ushirika namba 5 wa mwaka 2022, kuhusu uendeshaji wa mikutano kwa uwakilishi.

Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo, Mwl. Agness Keroka na Mwl. Fidelis Ngowi, wameishukuru bodi ya uendeshaji kwa kubuni njia bora za kukiendesha chama hicho, kwa madai kimekuwa kimbilio la watumishi na kupunguza adha za udhalilishaji kutoka kwa taasisi zingine za fedha.

Hata hivyo Mike Gafka, aliwahi kusema "Mafanikio ni kukubali changamoto zote utakazo kumbana nazo na si kuzikubali baadhi".

                          Mwisho.

0/Post a Comment/Comments