DCEA YAKAMATA DAWA ZA KULEVYA KG 3799.2

 


.............. 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya Kilogram 3799.22 za dawa za kulevya,pamoja na kutaifisha Mali za wahalifu wa dawa hizo zenye thamani ya Shilingi Bilioni tatu na Milioni mia tatu na nne. 

Akizungumza jijini Dar es salaam Kamishina Jenerali DCEA Aretas Lyimo amesema mafanikio hayo yanayokana na Operesheni mbalimbal ambazo wamezifanya mwezi Novemba mwaka huu ambapo pia wamefanikiwa kutekeleza ekari 19 za mashamba ya bangi na kuwakamata watuhumiwa 84 kuhusiana na dawa hizo.

Kamishina Jenerali Lyimo amesema kuwa Mahakama Kuu divisheni ya Rushwa na Uhujumi uchumi ilitoa maamuzi ya kutaifishwa kwa Mali zenye thamani ya Tsha Bilioni tatu na Milioni mia tatu na nne za watuhumiwa Saleh Basleman na Gawar Fakir kwa makosa ya kujihisisha na dawa za kulevya.

Akizitaja mali zilizotaifishwa Kamishna Jenerali amesema huo ni mkakati wa kuzuia uhalifu kuendelea na kuondoa matamanio ya kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali.


"Mali zilizotaifishwa zinajumuisha ni pamoja na Apartment QA2 Sea Breeze Residential Complex, Jangwani Beach ,Apartment 6B, Kariakoo,Nyumba mbili Mbezi, Kinondoni
Viwanja mbalimbali vya Mbweni, Kigogo (Kisarawell), Shungubweni, Boza na Bagamoyo,magomeni ,Apartment PA1 Sea Breeze Residential Complex Magari 11 yakiwemo Nissan Civilian, Subaru Impreza, Toyota Spacio na Volkswagen"amesema Kamishna Jenerali

Aidha Kamisha Jenerali Lyimo amesema katika Operesheni ambayo imefanyika katika eneo la Sinza Jiji la Dar es salaam iliwakamata Cuthbert Kalokola (34) na Bi.Murath Abdallah (19) wakiwa na dawa mpya ya kulevya. 

Hata hivyo Mamlaka hiyo imewataka watanzania kushiriki kwa pamoja katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za uhalifu wa dawa za kulevya.




0/Post a Comment/Comments