IGAD YASISITIZA USHIRIKANO KWA WADAU KATIKA MASUALA YA HALI YA HEWA.

Mwanasayansi wa utafiti wa Hali ya Hewa kutoka Kituo cha IGAD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi Titike Bahaga wakati akizungumza kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo imefanyika kwa siku tano kuanzia tar 8-12 Disemba mwaka huu katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.Afisa Mwandamizi ICPAC ambaye ni Mtaalamu anayesimamia nchi kumi na moja Afrika anayeangalia matumizi ya taarifa za hali ya hewa wakati akizungumza kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo imefanyika kwa siku tano kuanzia tar 8-12 Disemba mwaka huu katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.Meneja kutoka Shirika la Save the Children Mary Chavula akifuatilia kwa makini warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo imefanyika kwa siku tano kuanzia tar 8-12 Disemba mwaka huu katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.Washiriki kutoka sekta mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo wa pamoja kuhusu umuhimu wa taarifa za hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo imefanyika kwa siku tano kuanzia tar 8-12 Disemba mwaka huu katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.Mwanahabari kutoka SIFA FM ya nchini Kenya Linda Akothi akizungumza namna wanahabari wanashiriki katika kuelimisha jamii kuhusu taarifa za Hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo imefanyika kwa siku tano kuanzia tar 8-12 Disemba mwaka huu katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya (picha na Mussa Khalid)

...................

NA MUSSA KHALID, NAIVASHA KENYA 

Wawakilishi kutoka Huduma za Kitaifa za Hali ya Hewa (NMHSs),Mashirika ya Kiraia,sekta binafsi pamoja waaandishi wa habari wamesisitizwa kwenda kufanya taarifa na usambazaji wa huduma za taarifa za hali ya hewa ili kuisaidia jamii kuepukana na majanga.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwanasayansi wa utafiti wa Hali ya Hewa kutoka Kituo cha IGAD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi Titike Bahaga wakati akizungumza kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo imewakutanisha wadau katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.

Bahaga amesema kuwa malengo ya kuwakutanisha wadau hao ni kuwaongezea uelewa na utumiaji wa huduma za hali ya hewa kwa ajili ya ufuatiliaji wa hatari za kikanda, kutafsiri taarifa za hatari, na kusaidia mawasiliano na kufanya maamuzi.

"Tunaamini kwamba kama programu na mradi huu tunawekeza katika kutoa mafunzo kwa wanahabari kutoka vyombo mbambali ngazi ya kitaifa ikiwa ni kwa eneo muhimu la kueneza habari za hali ya hewa kwa jamii"

Kwa upande wake Mkufunzi wa wanahabari kutokea nchini Kenya Mr Issac Sagala lengo ni kupanga mikakati ya pamoja ili kuboresha ushirikiano na wadau kutoka katika sekta mbalimbali kupata taarifa zitakazosaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amewasisitiza wanahabari kudhibiti taarifa na kutoa taarifa ambazo zimethibitishwa na Mamlaka za Hali ya hewa ili kutoleta sintofahamu kwa jamii hasa za vijijini.

Katika warsha hiyo imejadiliwa namna na ushiriki na kuwalinda watoto katika masuala ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi ambapo Meneja kutoka Shirika la Save the Children Mary Chavula amesema kuwa wamefundisha ni kwa namna gani wazazi na jamii nzima wanapaswa kuwalinda watoto.

Amesema kuwa zimekuwa zikitumika mbinu mbalimbali za kuwafunza watoto ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari Radio,Tv na katika mitandao ya kijamii ili waweze kuwa vinara katika masuala ya hali ya hewa.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika warsha hiyo akiwemo Mwanahabari wa KIGALIINFO kutoka nchini Rwanda Saimon Kamuzinzi pamoja na Mwanahabari kutoka SIFA FM ya nchini Kenya Linda Akothi wamesema kuwa walichojinza ndio ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha habari wanazozitoa za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanawafaa zaidi wanaposhirikiana.

Aidha Linda amesema kuwa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi watoto wameathirika pakubwa hivyo warsha hiyo imeonyesha taswira kamili kuwa kuna uhitaji mkubwa wa washika dau kuwashirikisha ikiwemo kutengeneza habari zitakazowasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Warsha hiyo ya siku tano imeyakutanisha mataifa manne ya Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania,Rwanda,Burundi na Kenya ambao wamekuwa ni wenyeji imeratibiwa na Kituo cha IGAD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi (ICPAC), kwa ushirikiano na UK Met Office and Norwegian Capacity (NORCAP), kupitia mradi wa Uimarishaji wa Msimu wa Afrika Mashariki - Afrika Mashariki (PASS-EA) chini ya Mpango wa WISER Africa unaofadhiliwa na Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO) ambapo imelenga kuboresha ubora, ufikiaji, na matumizi ya taarifa za hali ya hewa.



0/Post a Comment/Comments