::::::::::::::
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewakamata watu waliokuwa wakijihusisha na uuzaji wa tiketi feki na nauli za kughushi katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli, Mbezi Luis, Dar es Salaam.
Hatua hiyo inakuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na LATRA kubaini udanganyifu katika kituo hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo, akizungumza wakati wa ziara ya kushtukiza katika stendi ya Mbezi Magufuli,amesema mawakala walikuwa wakitoza nauli kubwa kwa abiria na kuwapa tiketi zisizo halali.
Aliwataka abiria kuwa makini na kuchukua tiketi halali tu kutoka kwenye mifumo ya mtandao.
Mabasi yaliyojihusisha na udanganyifu wa nauli yamelazimika kuwapatia abiria fedha zao za ziada.
Katika hatua nyingine Cpa Suluo amewataka abiria kuhakikisha wanapata tiketi halali ili kuepuka hasara.
LATRA imetoa vibali 72 vya kuongeza mabasi ya muda ili kukabiliana na ongezeko la abiria. Mabasi 31 ni kwa ajili ya kituo cha Magufuli, na 41 kwa maeneo mengine ya nchi, ili kurahisisha usafiri katika kipindi cha sikukuu.
LATRA imewaelekeza abiria kulipa tiketi kupitia mifumo ya mtandao na kuthibitisha malipo kwa kutumia *LATRA App*. Pia, abiria wanapaswa kuwasiliana na LATRA kwa changamoto yoyote wanayokutana nayo.
Mawakala walikamatwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi baada ya kubainika kuhusika na uuzaji wa tiketi feki huku hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote wanaovunja sheria ili kuimarisha usalama wa abiria.
Mwisho.










Post a Comment