POLISI DAR YAPIGA MARUFUKU KUCHOMA MATAIRI NA KUPIGA BARUTI BILA VIBALI


...........

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharia wananchi wenye tabia ya kuchoma matairi barabarani na maeneo mengine hatarishi, kupiga baruti au fataki bila vibali maalum na kwa kufanya hivyo hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kundi lolote litakalobainika kufanya vitendo hivyo na kusababisha hofu au usumbufu kwa jamii.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema Jeshi la Polisi lina jukumu la kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya Mwaka Mpya, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Aidha,amesema kuwa Jeshi hilo  litaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi pia viongozi wa nyumba za ibada ili kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine.

Kamnda Muliro amesema Jeshi linaendelea kukumbusha maeneo ya makazi, ofisi na yale maeneo ya biashara kutoachwa wazi bila uangalizi katika kipindi cha sikuku na nyakati zingine, Polisi Dar es salaam inawatakia kila la kheri na kusherehekea kwa amani.

0/Post a Comment/Comments