Dar es Salaam
Bodi ya Maziwa Tanzania imewakutanisha wadau wa tasnia ya maziwa katika kikao kazi cha mwaka kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Msajili wa bodi hiyo, George Msalya, aliwataka wafanyabiashara wa maziwa kujisajili rasmi kabla ya kuendelea na shughuli zao.
Msalya alisema Sheria ya Maziwa Na. 8 ya mwaka 2004 inaipa bodi mamlaka ya kuwachukulia hatua wanaofanya biashara bila kufuata taratibu zilizowekwa.
Alieleza kuwa usajili unafanyika kupitia mfumo wa MIMS kwa njia ya mtandao, akionya kuwa kutosajiliwa kunaweza kusababisha kufungiwa biashara.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa kiwanda cha maziwa cha Kingolwira–Morogoro, Glorious Masawe, alisema vikao hivyo huongeza uelewa na kusaidia kuboresha mnyororo wa thamani wa uzalishaji.Afisa Masoko wa kiwanda cha maziwa cha Kingolwira–Morogoro, Glorious Masawe.






Post a Comment