NA MUSSA KHALID NAIVASHA,KENYA
Jumla ya washikadau kutoka sekta mbalimbali wakiwemo
waandishi wa habari kutoka mataifa manne ya Afrika Mashariki wamekutanishwa
nchini Kenya kwa lengo la kujadili umuhimu wa hali ya hewa na utekelezaji
katika kuzuia hatari na majanga yanayoweza kutokea.
Akizungumza kwenye warsha ya siku tano iliyoandaliwa na Kituo Cha IGARD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi (ICPAC) inayofanyika katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya,Afisa Mwandamizi ICPAC ambaye ni Mtaalamu anayesimamia nchi kumi na moja Afrika anayeangalia matumizi ya taarifa za hali ya hewa Collision Lore amezitaja nchi shiriki kuwa ni pamoja na Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Tanzania.
Lore amesema kuwa kwa sasa watu wanapokea htaarifa za
hewa lakini hawazitumiaa inavyotakiwa kwa kutoamini au kuamini hivyo ameeleza
ni muhimu kwa wadau wote kushirikiana katika kuzitua taarifa hizo kwa faida
katika kuisaidia jamii.
‘Changamoto kubwa inayotukuta sasa tunapeana taarifa za
hali ya hewa lakini uelewa kikamilifu bado haujaifiki ipasavyo katika ngazi za
vijijini kwani bado wananchi hawajapata uelewa kwa kuzitumia habari hizo
kikamilifu katika shughuli zao’amesema Lore
Lore amesema lengo pia ni kuimarisha ushirikiano kati ya huduma za kitaifa
za hali ya hewa, watunga sera, sekta binafsi, mashirika ya kiraia, na waandishi
wa habari katika kutumia, kuwasiliana, na kusambaza taarifa za hali ya hewa
zinazotolewa na ICPAC na NMHSs.
Lore ametumia fursa hiyo kusisitiza wadau kufanya kazi
kwa pamoja ikiwemo kutoa elimu ya matazamio ya hali ya hewa ili ujumbe huo
uweze kuwafikia watu wanaohusika ili waweze kujikinga na madhara ya mara kwa
mara.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Hali ya
Hewa nchini Kenya Mwai Zakari amesema kuwa wataendelea kushirikana na wadau
mbalimbali ili waweze kufahamu matumizi sahihi ya utabiri wa kila siku,wiki
mpaka mwezi uweze kuwasaidia katika shughuli zao.
Meneja wa ofisi kuu ya Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania Kantamla Mafuru amesema kutokana na kujifunza teknolojia mpya kwenye
mafunzo hayo yatasaidia kuwaongezea ujuzi kwenda kuchakata vizuri mifumo ya
hali ya hewa kuweza kujua matukio ya hali ya hewa ili kuijuza jamii matukio
yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika hafla hiyo
akiwemo Mwakilishi kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria Tanzania (Wizara
ya Afya) Dr Sijenunu Aroni amesema amejifunzo namna mabadiliko ya hali ya hewa
yanaweza kuathiri kuongezeka au kupungua kwa magonjwa hivyo inasaidia pia sekta
ya afya kuweza kujipanga kabla madhara hayajatokea.
Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji Tanzania Martin
Omego amesema mafunzo hayo yanasaidia kuonyesha mwanga kwa namna ambavyo
wanavyofanya shughuli za kila kwa kutumia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa.
Warsha hiyo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali imeanza kufanyika leo tar 08 -12 Disemba mwaka huu ambapo pia imetajwa kuwa ni itaendelea kufanyika Afrika ambapo itawakutanisha kwa pamoja Mataifa ya Ethiopia,Somalia,Sudan na Djibout.


Post a Comment