ZAIDI YA BILIONI 66.6 KUING'ARISHA CHATO


 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo, akitoa ufafanuzi

........

CHATO

HALMASHAURI ya wilaya ya Chato mkoani Geita inakusudia kukusanya na kutumia kiasi cha bilioni 66,619,120 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Serikali kuu, Halmashauri na wadau wengine wa maendeleo.

Hatua hiyo inakusudiwa kuing'arisha wilaya hiyo kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo pamoja na mishahara ya watumishi wa umma.

Aidha halmashauri hiyo inakusudia kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 5.3 kutoka vyanzo vyake vya ndani hali itakayosaidia kutatua,kuanzisha na kutekeleza baadhi ya miradi kiporo katika jamii.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita, Mandia Kihiyo, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Julai hadi Oktoba 2025 baada ya kutokuwepo kwa Baraza la Madiwani.

Itakumbukwa kuwa Madiwani wa halmashauri za wilaya, manispaa na Majiji walifikia kikomo cha uongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, hivyo kupisha uchunguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani nchini uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Katika taarifa yake kwa Baraza la Madiwani, Kihiyo amesema mbali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na vikao vilivyoketi, pia halmashauri hiyo imefanikiwa kuajili watumishi wapya 59 wa kada mbalimbali ili kupunguza uhaba wa watumishi katika halmashauri hiyo.

"Mwenyekiti mpaka sasa halmashauri yetu inao watumishi wa umma 3,811 katika vitengo tofauti na kwamba kwa kipindi ambacho hamkuwepo tumeajiri watumishi wapya 59 wa kada tofauti"amesema Kihiyo.

Kadhalika amedai kuwa baada ya kuapishwa kwa madiwani hao, halmashauri yake inakusudia kupokea vishikwambi kwaajili ya kuwagawia madiwani ili hatua itakayosaidia vikao vya Madiwani hao kwenda kisayansi ukilinganisha na zamani wakati wakitumia makabrasha.

                         Mwisho.

0/Post a Comment/Comments