DKT. KIJAJI AKUTANA NA TAASISI ZA WIZARA YAKE.

..........

Na Sixmund Begashe, Dodoma 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 14 Januari, 2026 ameongoza kikao kazi cha kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 zitakazojadiliwa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. 

Kikao hicho kinafanyika Mtumba Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, Managementi ya Wizara na viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizopo chini Wizara hiyo.







 

0/Post a Comment/Comments