KAPINGA, LONDO WAANZA SAFARI YA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA

 ameongoza watumishi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Waziri mpya, Mhe. Denis Londo  huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu ya wizara kwa maslahi mapana ya Taifa.

Akizungumza  katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, Mhe. Kapinga ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha Naibu Waziri Londo na kuelekeza Menejimenti pamoja na Watumishi wa Wizara kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo waliyojiwekea katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara nchini.

“Ninawahimiza Menejimenti na watumishi wote kushirikiana kikamilifu na Naibu Waziri ili kwa pamoja tuweze kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi na kufikia malengo ya Wizara kwa maslahi ya Taifa,” amesema Mhe. Kapinga.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), amesema kazi iliyo mbele yao ni kubwa na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ana matarajio makubwa kwao katika kusimamia sekta hiyo muhimu ya uchumi.

Aidha, Mhe. Londo amesema sehemu kubwa ya uzalishaji wa ajira nchini inatokana na sekta binafsi kupitia biashara na uwekezaji, huku akisisitiza kuwa dhima ya Dira ya Taifa ni kujenga uchumi jumuishi unaowashirikisha Watanzania wote.

“Tuna kazi kubwa ya kuwafanya Watanzania, hususan wa sekta binafsi, kutambua kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii na ujenzi wa Taifa. Tunahitaji kila mmoja aone ana nafasi na mchango katika kujenga Taifa letu,” amesema.

Amesema Wizara ya Viwanda na Biashara ina jukumu la kulea na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali, ili kuhakikisha kesho yao inakuwa bora zaidi kuliko walivyowakuta.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, amesema mafanikio ya sekta ya viwanda na biashara yanatokana na juhudi za pamoja za taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa uongozi thabiti wa Mhe. Judith Kapinga.

0/Post a Comment/Comments