SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA GEF KATIKA KULINDA MAZINGIRA

.....................

Dodoma

Serikali ya Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Mfuko wa Mazingira Duniani (Global Environment Facility, GEF) katika ajenda ya maendeleo ya taifa, hususan katika kuunga mkono juhudi za Serikali za uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa Dodoma Januari 30,2026 na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alipokutana na kufanya mazungumzo na Mashirika Wakala wa Mfuko wa GEF akieleza kuwa kupitia utaalamu, ushirikiano na taasisi za kitaifa, mipango ya uhifadhi ya Serikali mkono na GEF imeleta manufaa yanayoonekana ya kimazingira na kijamii na kiuchumi.

“Ushirikiano wetu umewezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika kushughulikia changamoto za mazingira, zikiwemo uharibifu wa ardhi, upotevu wa bioanuai, athari za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.

Ameongeza kuwa mengi yamepatikana chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hata hivyo, baadhi ya changamoto zimezidi kuongezeka na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha, kujenga uwezo wa kitaalamu pamoja ushirikishwa zaidi wa wadau kwa lengo la kupata matokeo makubwa zaidi.

Dkt. Muyungi amesema Serikali inathamini mchango unaotolewa na  mifuko hiyo na iko tayari kushirikiana zaidi na washirika ili kukusanya rasilimali nyingi zaidi, zinazolingana na ukubwa wa  changamoto zilizopo pamoja na matarajio ya kitaifa na kimataifa za mazingira ya uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Tunaposonga mbele, Serikali inatoa wito kwa Wizara, Taasisi na Mshirika wakala wa GEF kutumia nyanja mbalimbali kutoa taarifa ya mafaniko makubwa ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo uliopatikana kutokana na mchango wa Mfuko wa GEF. Vile vile ni wakati stahiki kwa wadau wote wa GEF kuongeza ushirikishwaji wa vijana katika utekelezaji wa miradi ya GEF ili kutumia ubunifu na utaalam walionao ili kuteta faida upande na uhifadhi na ustawi wa jamii kwa kuibua ajira za kijani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Farhat Mbarouk ameshukuru GEF kwa ushirikiano na Zanzibar kwa kuiwa miradi inayotekelezwa Zanzibar imekuwa chachu kubwa ya kuongeza juhudi za uhifadh sambamba na jamii kujipatika kipato kwa shughuli mbadala za kiuchumi ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa pamoja na utoaji wa elimu ya Uhifadhi na Utunzaji wa mazingira. Aidha, Mkurugenzi Farhat alisisitiza umuhimu wa kuongezwa kwa fedha za GEF upande wa Zanzibar ili kuibua miradi zaidi zaidi ya kuhifadhi mazingira na kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii na sekta za ukuaji wa Uchumi.




 

0/Post a Comment/Comments