MAVUNDE ATAKA USHIRIKI SEKTA YA MADINI

..................

Na Ester Maile Dodoma 

Serikali kupitia Wizara ya Madini imefanya marekebisho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini za mwaka 2018, kwa lengo la kuongeza ushiriki mpana wa Watanzania katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Hayo yamebainishwa leo Januari 05, 2026 Jijin Dodoma Na waziri wa Madini Antony Peter Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusuana na marekebisho ya kanuni katika sekta ya madini 

Ambapo marekebisho hayo yamefanyika kupitia Kanuni ya Kumi na Tatu (13), kifungu kidogo (A) ambacho kinahusu orodha ya bidhaa na huduma zinazotakiwa kutolewa na kampuni za Kitanzania zinazomilikiwa kwa asilimia mia moja (100%) na Watanzania. 

Hatua hii inalenga kuhakikisha Watanzania wanapata fursa zaidi za kiuchumi kupitia ajira, utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa katika shughuli za madini. 

Kwa awamu ya kwanza, tarehe 14 Novemba 2025, Tume ya Madini ilitangaza rasmi orodha ya bidhaa na huduma zinazopaswa kutolewa na kampuni zinazomilikiwa kwa asilimia mia moja na Watanzania. Orodha hiyo inatarajiwa kutoa mwongozo kwa migodi na wawekezaji katika kuzingatia kanuni za ushirikishwaji wa wazawa.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Serikali imewataka Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa kuhakikisha wanapata ujuzi na utaalamu unaohitajika katika shughuli za madini. Utaalamu huo utawawezesha Watanzania kustahili kupata ajira migodini pamoja na fursa za utoaji wa huduma mbalimbali katika miradi ya madini.

Aidha, Mavunde amewataka watoa huduma wote kuhakikisha wanazingatia viwango sahihi vya ubora, uaminifu na weledi katika utoaji wa huduma, ili kuongeza ushindani na kuimarisha mchango wa Watanzania katika sekta ya madini.

Hata hivyo Serikali imesisitiza kuwa ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini ni nguzo muhimu ya kukuza uchumi wa taifa na kuhakikisha manufaa ya rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania kwa ujumla.







0/Post a Comment/Comments