:::::::::::
Katika kuendeleza ushirikiano na wadau
wa Sekta ya Elimu nchini, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na
Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) wamefungua rasmi milango ya
utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali (WEMA), kwa lengo la kuboresha miundombinu ya elimu.
Kupitia ushirikiano huo, TEA na UNICEF
wametenga jumla ya shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa
vyumba vya madarasa, maabara za sayansi pamoja na matundu ya vyoo katika shule
20 ambapo, shule 11 zipo kisiwani Unguja na shule 9 kisiwani Pemba.
Akizungumza wakati wa kikao kazi maalum
cha kujadili utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha alisema, utekelezaji wa mradi unatarajiwa
kuanza mwishoni mwa mwezi Januari na kukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka
huu.
Dkt. Kipesha alibainisha kuwa lengo la
mradi huo ni kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora, salama na
rafiki kwa afya zao. Aliongeza kuwa TEA ni taasisi ya Muungano hivyo
utekelezaji wa miradi ya elimu Zanzibar ni sehemu ya majukumu yake ya msingi.
Aidha, alisisitiza kuwa ushirikiano
uliopo kati ya TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar umekuwa
nguzo muhimu ya mafanikio ya miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa na ambayo
imekamilika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Said, aliishukuru TEA kwa mchango
mkubwa kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu huku akieleza kuwa miradi hiyo
imekuwa kichocheo cha wadau wengine kujitokeza kusaidia maendeleo kwenye sekta
ya elimu.
Bw. Said aliongeza kuwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu hiyo umefika wakati muafaka kwani majengo mengi ya shule hizo ni ya kizamani na yako katika hali isiyoridhisha.
Alisema kukamilika kwa
miradi hiyo kutachangia kuinua kiwango cha taaluma kwani wanafunzi watapata
motisha ya kusoma katika mazingira ya kisasa.
“Wizara inatoa shukrani za dhati kwa TEA
kwa ushirikiano mkubwa mnaoendelea kutupatia katika kuboresha miundombinu ya
elimu na tunawaahidi kusimamia utekelezaji wa miradi yote kwa ufanisi ili ilete
tija kwa maendeleo ya sekta ya elimu,” alisema Bw. Said.
1. Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Said akifafanua jambo katika kikao kazi maalum cha kujadili utekelezaji wa miradi ya elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
1.
Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda akisistiza jambo kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na TEA kwa upande wa Zanzibar.
1. Baaddhi ya wataalamu kutoka TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia majadiliano kuhusu utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miundombinu kwenye shule za Unguja na Pemba unaotarajia kuanza Januari mwishoni 2026.
1. Muonekano wa maabara ya sayansi itayofanyiwa ukarabati katika shule ya Sekondari Chwaka iliyopo Wilaya ya Kati, Kusini Unguja.
Muonekano wa vyumba vya madarasa vitakavyofanyiwa ukarabati katika shule ya Sekondari CharaweWilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
1.
Muonekano
wa matundu ya vyoo yakayojengwa upya shule ya Sekondari Kijini iliyopo Wilaya
ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja
1
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment