Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imewahakikishia wakulima nchini upatikanaji wa mbolea ya kutosha katika msimu wote wa kilimo wa mwaka 2025/2026.
Mkurugenzi Mtendaji wa (TFRA) Joel Laurent, ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha kawaida cha waingizaji na wazalishaji wa mbolea nchini,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo.
Amesisitiza kuwa TFRA inaendelea kusimamia kwa karibu upatikanaji, ubora na usambazaji wa mbolea ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na kwa bei himilivu.
Laurent amesema kwa msimu huu wa kilimo, Mamlaka ilikadiria kutumia kiasi cha tani milioni moja za mbolea, na hadi kufikia Januari zaidi ya tani 981,542 sawa na asilimia 91 ya mahitaji zimeingizwa nchini, huku mbolea nyingine zikiendelea kuingizwa ili kukidhi mahitaji ya wakulima.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa tasnia ya mbolea, Wiliam Ngeleja Mjumbe wa Bodi, Kiwanda cha Mbolea Itracom, ameipongeza Mamlaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na kueleza vikao vinavyokutanisha wadau wa tasnia hiyo vinaongeza ufanisi katika utendaji wao wa siku kwa siku.
Aidha mmoja ya wadau katika kikao hicho Kisarika Nkya Mkurugenzi kutoka MwanaAfrika LDT amesema msimu huu wapo tayari kuendelea kushirikiana kama wadau ili kusapoti wakulima wadogo.
Hata hivyo Mkurugenzi
Mtendaji TFRA amesema kuwa mipango yao ni kuhakikisha matumizi ya mbolea katika
maeneo mbalimbali yanapatikana ili kumrahisishia mkulima kufanya kilimo chenye
tija.











Post a Comment