DKT. KIJAJI ATUA NYERERE, KUKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MIRADI YA KUENDELEZA UTALII KUSINI8

..........

Na Sixmund Begashe, Mtemere 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo Februari 10, 2026  ametua katika Kiwanja cha Ndege cha Mtemere kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere kukagua maandalizi ya uzinduzi wa miradi ya kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania. 

Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Mia moja imejengwa katika hifadhi za Taifa za Nyerere, Mikumi, Ruaha na Msitu wa Asili wa Kilimbero na inatarajiwa kuzinduliwa kesho februari 11, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere. 

Dkt. Kijaji, ameambatana na  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kigoma Malima, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, Menejimenti ya Wizara hiyo na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara.












0/Post a Comment/Comments