Bondia Fadhil Majiha amerudi kwenye ubora wake wa kuwa bondia namba moja nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa mtandao unaotunza na kutambua rekodi za mabondia Duniani, Boxrec unamtambua Majiha ndiye bondia namba moja kwa ubora wa jumla wote nchini Tanzania.
Pia Majiha amekua bondia namba moja katika uzani wake wa 'bantam'.
Na kwa upande wa Africa Majiha amekuwa namba tisa ambapo kwa jumla ya mabondia wote wa Tanzania yeye ndio kinara huku Mwakinyo akiwa wa 22.
Aidha Duniani, Majiha amekua kinara pia kwa kushika nafasi ya 291 kwa mabondia wote wa Tanzania huku Mwakinyo akiwa wa 503 katika orodha hiyo.
Majiha mwenye hadhi ya nyota nne alipanda ulingoni mnamo Januari 31 mwaka huu na kufanikiwa kumtandika kwa 'KO' bondia Harjot Singh wa India katika raundi ya kwanza ya pambano hilo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo kutoka katika mtandao huo wa ngumi Duniani, Majiha ndiye bondia namba moja wa Tanzania ambaye April mwaka huu anatarajiwa kupanda ulingoni kutetea taji lake la WBC Afrika.

Post a Comment