HIFADHI YA ZIWA DULUTI NI KWA MASLAHI YA TAIFA.



.............

Na Sixmund Begashe, Arusha 

Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika Uhifadhi wa Hifadhi ya Ziwa Duluti iliyopo Mkoani Arusha ili iendelee kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na taifa kwa ujumla. 

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt.  Ashatu Kijaji (Mb), kwenye Mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba (Mb) na wananchi wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha

Dkt. Kijaji amefafanua kuwa, Hifadhi ya Ziwa Duluti inatumika kwa shughuli mbalimbali za utalii zikiwemo, Utalii wa uvuvi (spot fishing), Utalii wa kutembea kwa Miguu, na utalii wa mandhari,  ambazo huingizia Serikali mapato. 

"Mathalani mwaka 2024/2025 jumla ya watalii 70,360 walitembelea hifadhi hiyo na kuingiza mapato ya shilingi 418,998,086 ,Alisema Dkt. Kijaji. 

Aidha amefafanua kuwa, sheria ya Misitu Sura 323 hairuhusu kufanya shughuli za kibinadamu kama vile uvuvi, kilimo, uchungaji na mifugo hivyo ni vyema wananchi wakaendelea kutoa ushirikiano wa kulinda Ikolojia katika Hifadhi hiyo ya kipekee nchini.

Fullshangweblog.co.tz 





 

0/Post a Comment/Comments