ICTC YASISITIZA WADAU KUSHIRIKI TUZO ZA TEHAMA 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa ya kufanyika Tuzo za TEHAMA 2026.
..................

NA MUSSA KHALID

Tume ya TEHAMA nchini (ICTC) kwa kushirikiana na wadau wa TEHAMA inatarajia kutoa tuzo ya TEHAMA 2026 ikiwa ni kutambua uvumbuzi, mabadiliko ya kidijitali, na ubora wa TEHAMA unaounda mustakabali wa taifa.

Akizungumza wakati akitambulisha ujio wa Tuzo hizo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga amewataja wadau shiriki kuwa ni pamoja na Chama cha Watoa huduma za Mtandaoni Tanzania (TISPA) na SophtVenture ambayo ni Kampuni ya Kitanzania inayoshughulika na ubunifu wa kiteknolojia,maendeleo ya Program na ushauri wa kidigitali.

Dkt Nkunde amesema kuwa Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Mwezi April mwaka huu zinalenga kutambua jitihada za kipekee zilzizofanywa na wadau wa TEHAMA na kutia hamasa katika maeneo mbalimbali ambayo TEHAMA inatumika ikiwemo huduma za kijamii,uzalishaji,utafiti,ubunifu,utawala na elimu.

Amesema tuzo zitakazotolewa zipo katika makundi mbalimbalki ambapo ni pamoja na  Uvumbuzi katika Bidhaa au Huduma za TEHAMA; Usalama wa TEHAMA – Usalama wa Mtandao na Ulinzi wa Data; Ubora na Mabadiliko ya Kidijitali; Kijana Mwenye Mafanikio katika TEHAMA; Wanawake katika TEHAMA; Matumizi Bora ya TEHAMA; TEHAMA katika Utangazaji, Vyombo vya Habari na Uandaaji wa Maudhui. 

Dkt Nkundwe Tuzo ya TEHAMA Endelevu; Tuzo za TISPA kwa Mtoa Huduma Bora za Mawasiliano; Tuzo za TEHAMA katika Utafiti, Uvumbuzi na Machapisho; TEHAMA kwa Watanzania waishio Nje ya Nchi (Diaspora); Tuzo za TEHAMA kwa Maendeleo; pamoja na Tuzo Maalum ya Utambuzi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SoftVenture Solutions Company Limited ambao ndio waratibu wa tuzo hizo Caroline Kombe amesema lengo lao ni kusimamia na kuhakikisha uwazi na uadilifu wa mchakato ikiwemo kusimamiza mawasiliano na uhamasishaji ili kufikia watu wengi zaidi.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama cha Watoa huduma za mitandao nchini (TISPA) Mzee Hamisi Boma amesema wataendelea kuwa washiriki wakubwa wa TEHAMA ili kuwafikia watumiaji wengi zaidi huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Deloitte na Kiongozi wa Kutoa Ushauri kwa TEHAMA Daniel Materu akisema lengo lao ni kuhakikisha tuzo hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia haki na uwazi.

Tuzo za TEHAMA ambazo dirisha limefunguliwa hadi tar 15 Machi mwaka huu ni muendelezo wa Tuzo za TEHAMA zilizofanyika kwa mara ya kwanza 2025 jijini Arusha hivyo wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali,watoa huduma pamoja nawawekezaji wametakiwa kutumia fursa ya kushiriki kwenye tuzo hizo.



0/Post a Comment/Comments