IDADI YA WAGONJWA JKCI YAONGEZEKA KWA WATU 4,943 MWAKA 2025

:::::::::

HOSPITALI ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group imetoa huduma za upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa wananchi 138,699 kwa mwaka 2025.

Akizungumza kuhusu takwimu hizo, Dkt. Shemu alisema idadi hiyo inaonyesha ongezeko la wagonjwa 4,943 ikilinganishwa na mwaka 2024 ambapo hospitali ilihudumia wagonjwa 133,756.

Alisema mwaka 2024 wagonjwa watu wazima walikuwa 109,931 na watoto 23,825, huku mwaka 2025 idadi ya watoto ikipungua na watu wazima kuongezeka.

Dkt. Shemu aliongeza kuwa mwaka 2025 hospitali hiyo ilianzisha huduma mpya ambazo hazikuwapo awali, zikiwemo upimaji wa shinikizo la damu kwa saa 24, uchunguzi wa umeme wa moyo kwa saa 24 na kipimo cha mishipa ya damu ya moyo kwa kutumia mashine ya treadmill.

Kwa upande wa upasuaji, alisema JKCI Hospitali ya Dar Group ilifanya upasuaji 1,874 mwaka 2025, ikijumuisha upasuaji wa mfumo wa mkojo, mifupa, uzazi, pua masikio na koo, matatizo ya wanawake pamoja na upasuaji wa jumla.





0/Post a Comment/Comments